Pages

mafundisho

Wednesday, August 10, 2011

Ombi la mwenye dhambi ni gani?



Swali: "Ombi la mwenye dhambi ni gani?"

Jibu: Ombi la mwenye dhambi ni Ombi ambalo mtu huomba kwa Mungu wakati anapotambua yakwamba yeye ni mwenye dhambi na anahitaji Mwokozi. Kusema Ombi hili la mwenye dhambi haikamilishi tayari kila kitu. Ombi la mwenye dhambi hufanya kazi tu sawasawa linapokuwa limesimamia kile mtu anacho fahamu, anacho elewa, na kukubali kuhusu dhambi zake na hitaji la Wokovu.

Hatua ya kwanza ya Ombi la mwenye dhambi ni kufahamu ya kwamba sisi sote ni wenye dhambi. Warumi 3:10 yasema hivi, “Kama ilivyoandikwa,ya kwamba,Hakuna mwenye haki hata mmoja.” Bibilia inaonyesha wazi ya kwamba sisi sote tumefanya dhambi. Sisi sote ni wenye dhambi na tunahitaji rehema na msamaha toka kwa Mungu (Tito 3:5-7). Kwa ajili ya dhambi zetu,tunastahili adhabu ya milele (Mathayo 25:46). Ombi hili la mwenye dhambi ni kwa kutafuta neema badala ya hukumu. Ni ombi la kuulizia rehema badala ya hasira kuu.

Hatua ya pili ya Ombi la mwenye dhambi ni kufahamu vile ambavyo Mungu amefanya kwa ajili ya kutibu hali ya upotevu wetu dhambini.Mungu alichukua mwili nakufanyika kuwa mwanadamu katika utu wa Yesu Kristo (Yohana 1:1,14). Yesu alitufundisha ukweli kuhusu Mungu na akaishi maisha makamilifu yenye haki na yasiyo kuwa na dhambi (Yohana 8:46; 2 Wakorintho 5:21). Yesu alikufa msalabani kwa ajili yetu, kwa kuchukua adhabu tuliyostahili (Warumi 5:8). Yesu alifufuka kutoka kwa wafu kudhihirisha ushindi wake juu ya dhambi,mauti,na jehanamu (Wakolosai 2:15; 2Wakorintho 15). Kwa ajili ya haya yote, tunaweza kusamehewa dhambi zetu na kuahidiwa uzima wa milele Mbinguni-tutakapo weka imani yetu ndani ya Yesu Kristo. Kile tunacho hitajika kufanya ni kuamini ya kwamba alikufa kwa ajili yetu na akafufuka kutoka kwa wafu (Warumi 10:9-10). Tunaweza kuokolewa kwa neema tu, kupitia imani peke yake, kwake Yesu pekee. Waefeso 2:8 yasema, “Kwa maana mmeokolewa kwa neema,kwa njia ya imani;ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu,ni kipawa cha Mungu.’’

Kusema Ombi hili la mwenye dhambi ni njia ya rahisi ya kumwelezea Mungu yakuwa unamtegemea Yesu Kristo kama mwokozi wako. Hakuna maneno ya kiuganga yenye kuleta wokovu. Ni kwa imani tu ndani ya kifo cha Yesu na kufufuka kwake vinavyo weza kutuokoa. Kama unafahamu yakwamba wewe ni mwenye dhambi na unahitaji wokovu kupitia kwa Yesu Kristo, hapa kunalo Ombi la mwenye dhambi unaloweza kuomba kwa Mungu: “Mungu, najua yakwamba mimi ni mwenye dhambi. Ninajua ya kwamba ninastahili adhabu ya dhambi zangu. Hata hivyo,ninamwamini Yesu Kristo kama mwokozi wangu. Ninaamini ya kwamba kifo chake na kufufuka kwake ilikuwa ni kwa ajili ya msamaha wangu. Ninamwamini Yesu na Yesu peke yake kama Bwana na Mwokozi wangu. Ahsante Bwana,kwa kuniokoa na kwa kunisamehe! Amina!’’

e, ina maanisha nini kuzaliwa mara ya pili kwa mkristo?

J

Swali: "Je, ina maanisha nini kuzaliwa mara ya pili kwa mkristo?"

Jibu: Je ina maanisha nini kuzaliwa mara ya pili kwa mkristo? Sehemu muhimu katika Bibilia inyo jibu swali hili ni Yohana 3:1-21. Bwana Yesu Kristo akizungumza na Nikodemo mkuu kati ya mafarisayo na mfuasi katika kikao (mahakama) kikuu cha wayahudi (Mfalme wa wayahudi). Nikodemo alikuwa amemjia Yesu usiku. Nikodemo alikuwa na maswali ya kumuuliza Yesu.

Wakati Yesu akizungumza na Nikodemo, alisema, Amin, Amin, nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Nikodemo akamwambia, “Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee?” “Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?” Yesu akajibu, “Amin, Amin, nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni Roho. Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, hamna budi kuzaliwa mara ya pili…” (Yohana 3:3-7).

Msemo “kuzaliwa mara ya pili” unamaanisha “zaliwa toka juu” Nikodemo alikuwa na uhitaji wa kweli. Alihitaji mabadiliko ya moyo wake... Mabadiliko ya kirohoUzao mpya, kuzaliwa mara ya pili, ni kitendo au hatua ya Kiungu ambapo uzima wa milele hupewa mtu yule aaminiye (2Wakorintho 5:17; Tito 3:5; 1Petro 1:3; 1Yohana 2:29; 3:9; 4:7; 5:1-4, 18). Yohana1:12, 13 inasema ya kuwa”kuzaliwa mara ya pili” pia ina maana “kufanyika mtoto wa Mungu”kwa imani katika jina la Yesu Kristo.

Swali hasa ni kuwa, “kwa nini mtu anahitaji kuzaliwa mara ya pili?” Mtume Paulo katika Waefeso 2:1 asema, “Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi …” Kwa Warumi katika Warumi3:23, Mtume aliandika, ”kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. “Kwahivyo mtu anahitaji kuzaliwa mara ya pili ili asamehewe dhambi zake na awe na uhusiano na Mungu.

Je, hii hutokea vipi? Waefeso2:8, 9 yasema, kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yoyote asije akajisifu.” Mtu anapo “okolewa”, basi yeye amezaliwa mara ya pili, akijazwa upya kiroho, na sasa amefanyika kuwa mwana wa Mungu kwa haki ya uzao mpya. Kwa kumwamini Kristo Yesu, yeye aliye adhibiwa kwa ajili ya dhambi alipokufa msalabani, ndiyo maana ya “kuzaliwa mara ya pili” kiroho. “Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya…” (2Wakorintho 5:17 a).

Kama bado hujaweza kumwamini Bwana Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako, je utakuwa na utayari wa kupokea Roho mtakatifu wakati akizungumza na moyo wako? Unahitaji kuzaliwa mara ya pili. Je, utaomba maombi ya kutubu na ufanyike kuwa kiumbe kipya ndani ya Kristo hivi leo? “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndiyo wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu” (Yohana 1:12-13).

Ukiwa unataka kumpokea Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako na uzaliwe mara ya pili, tazama mfano huu wa maombi. Kumbuka ya kwamba kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile haitaweza kukuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo pekee ndiko kutakuokoa toka dhambini. Ombi hili ni njia ya kumweleza Mungu imani yako kwake na kumshukuru kwa kukupea wokovu. “Mungu, najua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu na kwa msamaha-karama ya uzima wa milele! Amina!”

Biblia inasema nini juu ya kunywa kileo? Je, ni dhambi kwa mkristo kunywa kileo?

www.GotQuestions.org!
Swali: "Biblia inasema nini juu ya kunywa kileo? Je, ni dhambi kwa mkristo kunywa kileo?"

Jibu: Maandiko yana ilani nyingi juu ya kunywa kileo (mambo ya walawi 10:9; hesabu6:3; kumbukumbu la torati 29:6; waamuzi 13:4,7,14; samueli wa kwanza 1:15; methali 20:1; 31:4,6; isaya 5:11;22; 24:9; 28:7; 29:9; 56:12; mika 2:11; luka 1:15). Maandiko hayakatazi mkristo kunywa pombe, divai wala kinywaji chochote chenye kileo ndani. Maana maandiko mengine huzungumzia kileo kwa kuhalalisha matumizi yake. Mhubiri 9:7 inaamuru, “ kunywa kileo na moyo mkunjufu.” Zaburi 104:14-15 inaeleza Mungu hutoa divai “ inayofurahisha mioyo ya wanadamu.” Amosi 9:14 inazungumzia juu ya kunywa divai kutoka kwa shamba lako kama alama ya baraka za Mungu. Isaya 55;11 inapongeza “ naam, njoo ununue divai na maziwa…”

Kile Mungu anachowaamuru wakristo juu ya kileo ni wajizuie na ulevi (waefeso 5:18). Biblia inakataza ulevi na athari zake (methali 23:29-35). Wakristo wanakatazwa kuachilia miili yao itawalwe na vitu vinginevyo. (wakorintho wa kwanza 6:12; petro wa pili 2:19). Kunywa kileo kingi kunaathiri mtu. Maandiko yanakataza chochote kile ambacho kwa kukifanya unasababisha wengine kujikwaa( wakorintho wa kwanza 8:9-13). Kwa mujibu wa haya ni vigumu mkristo kukiri kuwa anakunywa kileo kwa utukufu wa Mungu ( wakorintho wa kwanza 10;31).

Yesu aligeuza maji kuwa Divai. Huenda ikawa Yesu alikuwa akinywa divai katika karamu Fulani Fulani (Yohana 2:1-11; Mathayo 26: 29). Katika nyakati za agano jipya, maji yalikuwa yakijawa na vidudu na uchafu kama hali ilivyo sasa katika mataifamengine ya ulimwengu wa tatu. Hii ndiyo sababu watu walipendelea kunywa divai kutoka kwa zabibu ili kuepukana na taka taka hizi. Katika timotheo wa kwanza 5:23, Paulo alimkataza timotheo kunywa maji yaliyokuwa yakimtatiza tumbo lake na mahali pake anywe divai. Divai ilikuwa na asili ya kileo ndani lakini haikuwa na kiwango cha kilevi sawa na cha leo. Haikuwa maji ya mzabibu moja kwa moja wala kileo sawa na cha leo. Maandiko hayakatazi mkristo kunywa kileo cha aina yoyote bali yanakataza ulevi na utumwa wa kileo (waefeso 5:18; wakorintho wa kwanza 6:12).

Kileo, kinapotumiwa kwa uchache hakina athari kwa mwenye kukitumia. Kutumia kiasi kichache cha kileo ni jambo linaloruhusiwa mkristo. Ulevi na utumwa wa kunywa kileo ni dhambi. Kwa sababu ya kushindwa kujizuia katika viwango vya matumizi ya kileo, kukwaza wengine na hata kupatikana na hatia mbali mbali, ni vizuri mkristo aepukane kabisa na matumizi ya kileo cha aina yoyote.