USIMZIMISHE ROHO MTAKATIFU
1thesaalonike 5:19 “usimzimishe Roho”
Maneno haya ni mawili tu yanayounda sentensi yenye uzito mkubwa sana. Ujumbe huu ni ujumbe ambao Paulo aliandika kwa Wathesalonike. Lakini Ujumbe huu unatufaa hata leo sisi tunaomngoja bwana harusi. Roho mtakatifu hukaa ndani yetu. Dhumuni lake ni kutiongezea nguvu roho ya mwanadamu maana mwili hushindana na roho na wala haiwezi kufanya inavyotaka, Kwahiyo roho zetu haziwezi bila Roho Mtakatifu. Ndipo Paulo akaliona hili na kuwaandikia kanisa lililoko THesalonike kwamba “wasimzimishe Roho”. Yawezekana hatujui kuwa sasa huyu Roho Mt. huzimika kwa jinsi gani. Kwa utafiti wa kibiblia nimeona kuwa zipo sababu ambazo ni hizi zifuatazo:-
Sababu zinazofanya Roho kuzimia:-
- Kutohudhuria kwenye ibada:
Mathayo 18:20 Neno la Mungu linasema wakusanyikapo wawili au watatu kwajili yake, Yeye Mungu yupo Pamoja nao.
Ibada: ni utaratibu wa kumuabudu Mungu na kumtolea sadaka.
- Kutotimiza matunda ya roho/kutoyafisha matendo ya mwili:
Galatia 5: 16-25. Basi nasema enendeni kwa roho wala hamtazitimiza taa za mwili. Ukiangalia hapo pia utaona matunda ya roho nay a mwili pia.
- Kuepuka kuwa kwazo:
Tunapokuwa makwazo kwa wengine tutasababisha utumishi wetu kulaumiwa. Hivyo ni vema kuepuka kukwaza wengine. 2wakorintho 6:3-6
- Kujichanganya na uasi/giza:
Wakiristo wengi wamekuwa wakisahau kuwa sisi ni nuru ya ulimwenngu na watu hututazama kila mahali. Sasa watoto wa Mungu tumekuwa tukihalalisha mambo ya dunia hii kuwa mengine yafafa kuigwa na wakristo. Shetani ametufunga macho hapo sana na kutufanya kutoulinganisha ulimwengu na Je neon la Mungu linasemaje juu ya hilo. Kiukweli kabisa watu wa Mungu tunaangamia kwa kukosa maarifa. 2wakorintho 6:14
- Kutokuwa na maombi:
1timotheo 2:1 Hapa Timotheo anasisitiza kwa habari ya kufanya dua, maombi, shukurani na sala zifanyike kwetu.
- Kutoshika neno la Mungu na kutolisoma:
1timotheo 1:13-14.
Kujifunza neno la Mungu ni vema kwakuwa ndio litupao maarifa na kutujenga katika ujasiri wa Kimungu.